Buha FM Radio
Buha FM Radio
January 22, 2026, 11:30 am

Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu imefanikiwa kukusanya zaidi ya Bilion 20.8 sawa na asilimia 54 kwa bajeti ya mwaka wa Fedha 2025/2026 huku ikijipanga kukusanya Bilion 44.7 mwaka wa fedha 2o26/2027.
Na Sharifat Shinji
Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma imefanikiwa kukusanya zaidi ya bilioni 20.8 kutoka Ruzuku ya Serikali, wadau wa maendeleo na vyanzo vya mapato ya ndani ya Halmashauri Sawa na asilimia 54 kwa bajeti ya mwaka wa Fedha 2025/2026.
Akisoma taarifa ya mapendekezo ya mpango na bajeti ya mapato na matumizi pamoja na miradi ya maendeleo kwa mwaka 2026/2027 Mkuu wa Divisheni ya Mipango na Uratibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Bw. Samweli Sendegeya amesema Halmashauri ilikadiria kukusanya na kutumia Bilioni 38.2 kwa mwaka wa Fedha 2025/2026.
Aidha Bw. Sendegeya amesema Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu imekusanya Bilioni 3.2 kutoka mapato ya ndani sawa na asilimia 76 ambapo Halimashauri ilikadiria kukusanya zaidi ya Bilioni 4.3 kutoka vyanzo vya ndani kwa mwaka 2025/2026.
Kwa upande wao baadhi ya wajumbe waliohudhulia kikao hicho cha kuwasilisha mapendekezo ya mpango na bajeti ya mapato na matumizi pamoja na miradi ya maendeleo kwa mwaka 2026/2027 wamesema bajeti iliyopendekezwa inapaswa kusimamiwa ili iweze kuleta tija katika Halmashauri ya wilaya ya Kasulu.

Hata hivyo Halimashauri ya Wilaya ya Kasulu imekusudia kukusanya Zaidi ya Bilioni 44.7 kwa mwaka wa Fedha 2026/2027 ambapo kati ya bilioni 27.9 ni fedha ya mishahara, bilioni 10.3 fedha ya miradi ya maendeleo, Bilioni 1.5 matumizi ya Ruzuku ya Serikali huku 4.8 ni mapato ya ndani ya Halmashauri.