Buha FM Radio
Buha FM Radio
January 8, 2026, 5:02 pm

Mvua za masika zatajwa kusababisha mzorotesha biashara ya viatu katika maeneo mbalimbali ikiwemo genge la Kwashayo katika Halmashauri ya Mji Kasulu.
Na; Emily Adam
Wafanyabiashara wa Viatu malufu Ndala na Yeboyebo katika genge la Kwashayo Halmashauri ya Mji Kasulu mkoani Kigoma wameeleza changamoto ambazo wanakumbananazo kwenye shughuli zao huku wakitaja msimu wa masika wateja hupungua tofauti na kiangazi.
Bila Juma ameongea na Buha FM radio kwa niaba ya wafanya biashara wenzake, amesema kukosa wateja katika msimu wa masika ni kutokana na bidhaa hizo kupanda katika masoko yao hali inayopelekea wateja kushindwa kwenda na hali ilivyo sokoni.
Aidha amesema kupanda bei ya bidhaa hizo imetokana na uhaba wa malighafi viwandani pamoja na gharama ya usafirishaji wakati wa masika huwa ni changamoto kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kutoa ushauri kwa viajana kuendelea kujishughulisha na kazi halali.
Katika hatua nyingine wafanya biashara hao wanakabiliwa na changamoto wa ubovu wa miundombinu ya kufanyia biashara ambapo wanalazimika kuuzia pembezoni mwa barabara wakitaja kuwa ndo eneo pekee linalofikiwa na wateja kwa wakati.