Buha FM Radio
Buha FM Radio
October 8, 2025, 5:55 pm

“Tutaendelea kuwashirikisha uzuri mkuu wa Wilaya yetu ni mdau wa michezo hivyo sisi tutaendelea kuwasapoti katika maswala ya michezo na hatutakomea hapa ni mwendelezo na sehemu nyingine wajianadaa na mlioshinda hapa mtarajie mazuri kwenda kushiriki sehemu nyingine” Amesema Mtewele.
Na; Sharifat Shinji
Serikali ya Wilaya ya Kasulu chini ya mkuu wa Wilaya hiyo Kanal Isac Mwakisu imeendelea kuunga mkono na kushirikiana na wadau katika kuwawezesha vijana kuinua vipaji vyao katika michezo mbalimbali ikiwemp mpira wa miguu kwa upande wa wanaume na wasichana wilayani humo.
Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Pamba Dunia yaliyofanyika Ocktoba 7, 2025 katika Kata ya Asante Nyerere katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Katibu Tawala Wilaya hiyo Bi. Telesia Mtewele amesema Serikali ya Wilaya na Kampuni ya ununuzi wa Pamba wilayani Kasulu NGS chini ya Mkuu wa Wilaya wanaendelea kuunga mkono masuala ya michezo wilayani humo.
Tukio la Maadhimisho ya siku ya Pamba Duniani liliambatana na mchezo wa mpira wa Miguu kati ya timu mwenyeji Intozi Fc kutoka kata ya Asante Nyerere dhidi ya Rungwe City Combain kutoka kata ya Rungwe Mpya ambapo mchezo huo ulimalizika kwa Intozi Fc kupoteza kichapo 1-0 katika dimba la Shule ya msingi Asante Nyerere huku Kocha wa timu ya Rungwe City Yusuph Zabron akieleza furaha yake na mbinu alizozitumia kupata matokeo hayo katika uwanja wa ugenini huku akisisitiz vijana kujituma na kuonesha vipaji vyao ili kufikia malengo yao.

Kwa upande wa timu mwenyeji nahodha wa Intozi FC Elias Luvumbaga amezungumzia namna mchezo ulivyokuwa na kuahidi kuwa wataendelea kurekebisha katika michezo mingine huku akiomba serikali kuendelea kuwafikia watu wa vijijini ili kuibua vipaji walivyonavyo na kufikia ndoto zao.

Hata hivyo imekuwa mwendelezo kwa Uongozi wa Wilaya ya kasulu kuwapa nguvu vijana katika masuala ya michezo kama alivyoeleza Katibu Tawala Septemba 6, 2025 Ofisi ya Mkuu wa Wilaya iliandaa Bonanza la maandalizi ya Mbio za Mwenge wa uhuru 2025 ambapo lilihusisha michezo mbalimbali katika uwanja wa Kiganamo katika Halmashauri ya Mji Kasulu.
