Buha FM Radio
Buha FM Radio
October 8, 2025, 3:37 pm

Wakulima wa kilimo cha Pamba wamejitokeza kushiliki Maadhimisho ya siku ya Pamba duniani ambapo katika Wilaya ya Kasulu yamefanyika kata ya Asante Nyerere huku mamia ya wananchi wakijitokeza kwa wingi kushudia zoezi hilo.
Na; Sharifat Shinji
Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma imetumia Zaidi ya Bilion 3 katika kilimo cha Pamba Kwa misimu mitano ya kilimo kuanzia msimu wa mwaka 2020/2021 hadi msimu wa mwaka 2024/2025 kwa ajili ya ununuzi wa pemejeo za wakulima wa zao hilo.
Akizungumza leo Mkaguzi wa Pamba Wilaya ya Kasulu Ndg. Michael Kihiga Wakati wa kuwasilisha Taarifa katika maadhimisho ya siku ya Pamba duniani iliyofanyika Kata ya Asante Nyerere Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma na kusema msimu wa 2025/2026 wanatarajia kulima Hekari 12,350.

Aidha Ndg. Kihiga amesema msimu huu wamepanga kusambaza pembejeo kwa wakulima wote pamoja na kutoa elimu ya matumizi sahihi ya pembejeo hizo na kuhamasisha kilimo kwa kila kaya ya wakazi wa wilaya ya kaulu.
“ Msimu huu wa kilimo tumejipanga kusambaza Tani 150 ya mbegu kwa wakulima wote, tutasambaza viuwadudu Hekapark 72,210, pampu/vinyunyizi 500 pia kwa kushirikiana na Wilaya ya Kasulu tutaendelea kutoa elimu ya matumizi ya viuwadud, vinyunyizi, na matumizi ya mbegu na mbolea ili kuendeleza kilimo cha Pamba katika Wilaya yetu ya Kasulu” Amesema Kihiga.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Isack Mwakisu amesema ufumbuzi wa changamoto ya wadudu waharibifu katika zao hilo ukitatuliwa utaleta tija kwa wakulima wa Kasulu na mkoa wa Kigoma kwa ujumla huku akimalizia kwa kuzindua msimu wa Kilimo cha Zao la hilo kwa mwaka 2025/2026 katika Wilaya Kasulu na Mkoa kwa ujumla.

Kanali Mwakisu ameongezea kwa kuwapongeza adau wa Pamba pamoja na wakulima wa zao hilo na kuwaomba wakazi wa Kasulu kujiunga katika shughuli za kilimo cha zao la Pamba ili kusaidia kuendelea kuhifadhi mazao ya chakula kwa ajili ya chakula na Zao la Pamba kulitumia kwenye Biashara.
“Mategemeo yangu ni kuwa mtaendelea kuhamasika na kilimo cha Pamba ili kuleta tija na kuleta uchumi endelevu, changamoto iliyosemwa hapa ni uchache wa wakulima wa zao hili hivyo kupitia maadhimisho haya wananchi tulime Pamba ili mazao ya mahindi na maharage yabaki kwa ajili ya Chakula” Amesema Kanali Mwakisu.
Katika hatua nyingine Baadhi ya wakulima wa zao hilo akiwemo Mipawa Jilala, Edisa Mtogwa na Bulolo Majenga wameshukuru na kueleza namna ambavyo wamejipanga kuendeleza kilimo cha Pamba kwa msimu huu kuku wakiiomba serikali kuwapatia pembejeo kwa njia lahisi ili waweze keendeleza kilimo hicho.
Maadhimisho ya siku ya Pamba Duniani huadhimishwa kila mwaka ifikapo oktoba 7 ambapo kwa mara ya kwanza Wilaya ya Kasulu na mkoa wa Kigoma kwa ujumla imeadhimisha siku hiyo ikilenga kuongeza uzalishaji wa zao la Pamba kupitia kilimo huku kauli mbiu ya Maadhimisho hayo ikiwa ni “Pamba ni fahari ya maisha na mazingira yetu,shiriki uchaguzi mkuu2025 kwa amani na utulivu”
