Buha FM Radio

Wazee Kasulu wataja changamoto zinazowakabili

October 3, 2025, 10:28 am

Meza kuu katika maadhimisho ya siku ya wazee duniani katika Halmashauri ya Mji Kasulu. Picha na Irene Charles

Wazee Katika Halmashauri ya Mji Kaasulu walia na serikali kukabiliana na uonevu wanaoupitia katika maishayao ya kawaida.

Na; Emily Adam

Baadhi ya wazee katika Halmashauri ya Mji Kasulu mkoani Kigoma wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa huduma bora ya matibabu, umasikini, unyanyapaa pamoja na kunyanganywa mali zao kama vile ardhi na vitu vingine.

Wamebainisha hayo wakati wakizungumza na Buha FM radio katika maadhimisho ya siku ya wazee Duniani katika Ofisi za Halmashauri ya Mji Kasulu na kuomba serikali kuwasaidia kutatua changamoto hizo.

Baadhi ya sauti za wazee katika Halmashauri ya Mji Kasulu.

Kwa upande wake mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu katika kilele cha siku hiyo Sabinus Chaula amesema ipo haja ya kutoa elimu ya kuwatunza na kutatua changamoto hizo huku akiwahimiza kujiunga na kujisajili katika vikundi ili wapate mikopo ya asilimia 30% inayotolewa na Halmasauri.

Sauti ya mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu Ndg. Sabinus Chaula.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasul Ndg. Sabinus Chaula. Picha na Irene

Naye mratibu wa Asasi ya Wakwanza Paralegal organization linalojishughulisha na kutoa huduma za kisheria kwa wananchi Nyandwi Kleofas amesema wamekuwa wakishirikiana na maafisa ustawi wa jamii kutatua baadhi ya changamoto zinanowakabili wazee ambapo amewaasa kutumia msaada wa kisheria.

Sauti ya mratibu wa Asasi ya Wakwanza Paralegal organization Nyandwi Kleofas.

Oktoba mosi kila mwaka Dunia huadhimisha siku ya wazee duniani ambapo ilianzishwa mwaka 1990 na Umoja wa Mataifa huku lengo kuu ni Kutambua mchango wa wazee katika jamii, Kuelimisha jamii kuhusu changamoto zinazowakabili pamoja na kuhamasisha ushiriki wa wazee katika maendeleo ya jamii.

Baadhi ya wazee katika Halmashauri ya Mji Kasulu mkoani kigoma katika maadhimisho ya Wazee duniani. Picha na Irene Cherles.