Buha FM Radio
Buha FM Radio
August 13, 2025, 11:21 am

“Pombe ina athari kwa mama mjamzito moja kwa moja hasa anayetumia lakini pia sigara ina madhara makubwa haijalishi anavuta au havuti hivyo wajawazito hawatakiwi kuvuta au kutumia pombe wakati wa ujauzito kwani inaweza kuathiri mtoto aliyepo tumboni” Amesema Dkt. Ally.
Na; Irene Lucas
Ili kupata mtoto mwenye afya njema mama mjiamzito hapaswi kutumia pombe wala kuvuta sigara ili kuepukana na madhara yanayoweza kumpata mtoto pamoja na mama mwenyewe.
Hayo yamebainishwa leo kupitia kipindi cha shangwe la asubuhi na mtaalamu wa maswala ya uzazi Dkt. Ally Msafiri Kutoka hosptali ya mlimani wilayani Kasulu amesema mtoto kuzaliwa amefariki, kuwa na kichwa kidogo, ulemavu na uwezo wa kufikiria ni baadhi ya athari zinazotokana na matumizi ya pombe na sigara.
Aidha Dkt. Ally amesema madhara hayo yatajitokeza mwanzoni mwa ujauzito kama mama akiwa na kunywa pombe na kufuta sigara wiki tano au sita kabla ya kutarajia kupata ujauzito.

Dkt Ally ameongeza kuwa kwa mwaume au kwa mtu yoyote anayetumia sigara anaweza kusababisha madhara ya moja kwa moja kupitia moshi wa sigara akiwa anavuta karibu na mama mjamzito hivyo kutapa shida ya kifua.
Dkt. Ally amesema mtu anaweza kuacha kutumia kwa kufuata ushauri wa wataalamu wa afya, kukaa na kuongea na watu unaowaamili wanaoweza kushari mazuri, kutokaa na watu wanaotumia pombe, kutumia dawa za kupunguza athari.
Agosti 5 mwaka 2024 BBC ilichapisha kuwa zaidi ya miaka 50, wanasayansi wameonya juu ya hatari za kunywa pombe wakati wa ujauzito. Utafiti wa hivi karibuni umegundua kuwa unywaji pombe hata mara moja kwa wiki, unaweza kuathiri ukuaji wa ubongo wa mtoto, ufahamu na tabia zake, na sura ya uso.
