Buha FM Radio
Buha FM Radio
July 24, 2025, 10:28 pm

Kuna aina tatu za mbolea ambazo ni mbolea za Samadi (kinyesi cha Mnyama au ndege) ambazo zinamatikana kwa urahisi majumbani, Mbolea zinazotoka viwandani na mbolea inayotokana na masalia ya mimea, mabaki ya samaki pamoja na mifupa ya ndege.
Na Irene Charles
Kila mkulima ana jukumu la kujua ni mbolea gani anapaswa kutumia shambani ambayo italeta matokeo mazuri na kusaidia kizazi na kizazi kutumia ardhi hiyo na si kila mbolea na inapaswa kuwekwa shambani.
Hayo yamesemwa leo na Afisa kilimo Prof. Masanja wakati akizungumza na Buha FM Redio na kusema mkulima anapaswa kufahamu ni aina gani ya mbolea anatumia kulingana na ardhi yake kwa lengo la kulinda ardhi hiyo.
Aidha Prof. Masanja amewashauri wakulima kutumia mbolea kiasi cha mfuko wa kilo 50 kwa kupandia na mfuko wa kilo 50 kwaajili ya kukuzia mazao kwa ekari moja lakini kwa mkulima wa nyumbani kifuniko kimoja cha maji kwa kila shina.
Hata hivyo Prof. Masanja amesema mkulima ambaye hatatumia mbolea ambayo sio sahihi atasababisha uharibu wa aridhi lakini pia mmea kudhohofika na hivyo kupata mavuno kwa kiwango cha chini.
Kwa mujibu wa Prof. Masanja kuna aina tatu za mbolea ambazo ni mbolea za Samadi (kinyesi cha Mnyama au ndege) ambazo zinamatikana kwa urahisi majumbani, Mbolea zinazotoka viwandani na mbolea inayotokana na masalia ya mimea, mabaki ya samaki pamoja na mifupa ya ndege.