Buha FM Radio

Halmashauri ya Mji Kasulu yasisitiza kutunza mazingira

June 5, 2025, 11:11 pm

Pichani ni Afisa mazingira katika halmashauri ya mji Kasulu Ndg. Wambura Muniko akiwa katika studio za Buha FM radio wakati wa mahojiano kuhusu mazingira. Picha na Sharifat Shinji.

Afisa Mazingira na Kaimu kitengo cha MaliaSili na Ujifadhi wa Mazingira katika Halmashauri ya Mji Kasulu Ndg. Wambura Muniko amewaomba wakazi wa halmashauri ya Mji huo kuendelea kuyatunza mazingira ili kuepuka mabadiliko ya tabianchi yanayoweza kujitokeza baada ya mazingira kuathirika.

Na: Sharifat Shinji

Kila tarehe 5 Juni, kila mwaka Tanzania inaungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani. Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliamuliwa na Baraza la Umoja wa Mataifa la mwaka 1972, wakati wa mkutano wa kwanza wa Umoja wa Mataifa uliohusu Mazingira huko Stockholm, nchini Sweden.

Madhumuni ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ni kuhamasisha jamii duniani kote kuelewa masuala yahusuyo Mazingira na pia kuhamasisha watu wa jamii mbalimbali duniani kuwa mstari wa mbele katika kuchukua hatua za kuhifadhi na kulinda mazingira.

Hivyo kupitia Buha FM radio Halmashauri ya Mji Kasulu imeendelea kuwakumbusha wananchi kuendelea kuyatunza mazingira na kuepuka utupaji taka katika vyanzo maji na sehemu zingine bali kufata utaratibu ambao Halmashauri imeuweka katika kuhakikisha Mji wa Kasulu unabaki kuwa msafi.

Pichani ni Afisa mazingira katika halmashauri ya mji Kasulu Ndg. Wambura Muniko akiwa katika studio za Buha FM radio wakati wa mahojiano kuhusu mazingira. Picha na Sharifat Shinji.