Buha FM Radio
Buha FM Radio
April 24, 2025, 2:51 am

Katibu tawala Bi, Theresia Mtewele awapongeza waote walioshiriki zoezi la usafi katika maeneo yote wilayani Kasulu.
Katika kuadhimisha miaka 63 za Uhuru wa Tanganyika Leo Decemba 9 Buha fm radio ilifika katika Hospital ya Halmashauri ya Mji Kasulu ambako kulikuwa na zoezi la usafi wa mazingira ikiwa ni sehemu ya Utekerezaji wa akizo la Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhusu kuadhimisha siku ya Uhuru wa Tanganyika
Katibu tawala wa wilaya ya Kasulu Bi, Theresia Mtewele Ameshiriki katika zoezi la usafi katika Hospitali Ya Halmashauri ya Mji Kasulu huku akipongeza zoezi hilo baada kukamilika.

Aidha Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Kasulu Mwalimu Vumilia Simbeye amezungumza mara baada ya Zoezi la usafi katika hospitali hiyo huku akisema zoezi hilo ni kuboresha mazingira hospitali hiyo.

Kwa Upande wa Jeshi la polis wilaya ya kasulu limeshiriki katika zoezi hilo huku Mkuu wa Jeshi la Polisi SSP SANGO amesema jeshi la polisi linajukumu la kushirikiana na wanachi katika zoezi hilo ili kuweka mazingira salama.
Zoezi la usafi limefanyika katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji Kasulu likiwa na kauli Mbiu ya UONGOZI MADHUBUTI NA USHIRIKISHWAJI NDO MSINGI WA MAENDELEO YETU ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru wa Tanaganiyika huku Halmaashauri ya Kasulu vijijini zoezi hilo limefanyika katika Hospitali ya wilaya hiyo likiwa limeambatana na uchangiaji wa Damu.
