Unyanja FM
Viongozi wa shule wapewa mafunzo ya manunuzi
September 11, 2023, 9:46 am
Walimu wa shule za msingi na sekondari wilayani Nyasa wapatiwa mafunzo kuhusu manunuzi ya umma.
Na Sichali Netho
Halmashauri ya wilaya ya Nyasa Septemba 9, 2023 imetoa mafunzo ya mfumo wa manunuzi wa umma (NeST) kwa wataalam kutoka shule za msingi, sekondari na afya.
Lengo la mafunzo ni kuwajengea uwezo jinsi ya kuandaa mpango wa manunuzi kutoka katika idara zao.
Mafunzo yanafanyika shule ya msingi Kilosa Kwa Tarafa ya Ruhekei.