Veta Nyasa Fursa kwa kujiajiri
December 3, 2024, 11:39 am
Chuo cha Ufundi Stadi Veta Nyasa kimefanya Mahafali yake ya kwanza mahafali yaliyofanyika hivi karibuni katika Viwanja vya Chuo hicho na Mgeni Rasmi katika Mahafali hayo ni Mkuu Wa Wilaya ya Nyasa Mhe. Peres Magiri .
kwenye picha ni mgeni rasmi ambae ni mkuu wa wilaya ya nyasa akipokea maelekezo kutoka kwa mwanafunzi wa veta namna ya kutumia mitambo ya ujenzi
Chuo cha Ufundi Stadi Veta Nyasa kimefanya Mahafali yake ya kwanza mahafali yaliyofanyika hivi karibuni katika Viwanja vya Chuo hicho na Mgeni Rasmi katika Mahafali hayo ni Mkuu Wa Wilaya ya Nyasa Mhe. Peres Magiri .
Mhe. Magiri amewataka wananchi wa Wilaya ya Nyasa kusoma chuo cha VETA Nyasa kwa lengo la kupata ujuzi utakaowasaidia kujiajiri, na kuongeza kipato kwa mtu mmoja, kaya na Taifa kwa ujumla. Uwezo wa Chuo hiki ni kuchukua wanafuznzi zaidi ya 160, lakini mpaka sasa chuo hiki kinadahili wanafunzi 80 hivyo basi tunatakaiwa kutumia fursa hii kupata ujuzi.
Aidha amewasihi wahitimu kwenda vijijini na kutumia ujuzi wao kwa kuanzisha vikundi kwa kufanya shughuli walizosomea na Serikali itawaunga mkono kwa kuwakopeshha Asilimia kumi ya mapato, badala ya kwenda mijini kupoteza muda.
pichani mkuu wa chuo cha veta Nyasa
Awali Mkuu wa Chuo hicho Fortunata Shiyo ameiomba Serikali kuendelea kuboresha miundombinu ya Umeme kwa kuwa kuna mashine za kisasa zinazotumia umeme mwingi zaidi ombi ambalo limepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Nyasa na limeanza kufanyiwa kazi.Aidha amewataka wazazi walezi kuwaleta wanafunzi katika chuo hicho kwa kuwa bado kinanafasi za kutosha kuwapa ujuzi wakazi wa Wilaya ya Nyasa.
sauti ya mkuu wa chuo cha veta