Takukuru Nyasa yatoa elimu kupambana na rushwa kuelekea uchaguzi selikali za mitaa
August 16, 2024, 10:29 pm
Taasisi ya kuzui na kupamba na rushwa (TAKUKURU) wilaya ya nyasa mkoani Ruvuma inaendele na zoezi la kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kupiga vita vitendo vya rushwa wakati taifa likielekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
Akizungumza na waandisha wa habari hii leo kamanda wa TAKUKURU wilaya ya nyasa JUMANNE IZIMBULE amesema serikali inapata mamlaka yote kutoka kwa wananchi kwa njia ya uchaguzi vitendo vya rushwa katika michakato ya uchaguzi vinapaswa kupingwa vikali na wananchi kwa kushirikiana na taasisi husika ili kupata viongozi weledi ambao watawatumikia wananchi.
sauti ya jumanne izimbule
Hata hivyo ametaja baadhi ya madhara yatokanayo na rushwa kwenye uchaguzi ikiwemo kuchagua viongo wezi na wabadhilifu wa mali za umma, pamoja na kudumaa kwa demokrasia ya nchi.
sauti ya jumanne izimbule
Pamoja na mambo mengine amewataka waandishi wa habari na watanzania wote kwa kila mmoja wetu kujua kwamba anawajibu wa kuzuia na kupambana na rushwa huku akitaja namba 113 kwamba mtu yeyeto mwenye taarifa ya kitendo chochote kinachohusisha rushwa apige simu namba 113 bure
Kwa mujibu wa tume huru ya taifa ya uchaguzi INEC imetoa ratiba ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu kwamba uchaguzi utafanyika Tarehe 27 November 2024 kabla ya tarehe ya uchaguzi zitafanyika shughuli zingine ikiwemo zoezi la uandikishaji wapiga kura,kuchukua fomu za kugombea, kufanyika kwa kampeni za uchaguzi.