Savvy FM
Savvy FM
December 18, 2025, 6:26 pm

Meya wa Jiji la Arusha, Maximilian Iranghe, amesema ziara ya Waziri wa tamisemi, Riziki Shemdoe, mkoani Arusha imelenga kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa jijini humo, ikiwemo ujenzi wa uwanja wa mpira na ujenzi wa soko.
Na Mariam Malya
Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake, Meya Iranghe amesema waziri ameridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo, huku akisisitiza kuwa hakuna sababu ya kuongeza muda wa utekelezaji wa miradi iliyopangwa.
Aidha, kwa upande mwingine, Meya Iranghe ametoa shukrani kwa Waziri wa Ujenzi kwa kutembelea miradi hiyo, akisema ziara hiyo ina manufaa makubwa kwa Jiji la Arusha kwani inasaidia kusukuma mbele kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.