Savvy FM

Baraza la Madiwani Arusha lazinduliwa, DC Mkude ateta

December 4, 2025, 5:37 pm

Meya wa jiji la Arusha Maximilian Iranghe akizungumza wakati wa uzinduzi wa baraza la madiwani. Picha na Mariam Mallya

Mkutano wa kwanza wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Arusha umezinduliwa leo, tarehe 4 Desemba 2025, katika ukumbi wa Mkuu wa mkoa wa Arusha.

Na Mariam Mallya

Kabla ya uzinduzi huo, madiwani wote walikula viapo vya uadilifu kama ishara ya kuanza rasmi majukumu yao ya kiuongozi.

Sauti za madiwani wakilakiapo

Katika uchaguzi wa nafasi ya Naibu Meya, jumla ya madiwani 34 walipiga kura halali. mgombea kutoka chama cha NLD, Collins Nathani Stanley, akipata kura 3, huku mgombea wa CCM, Julius Medeye, akipata kura 31 na kuibuka mshindi. Matokeo hayo yalitangazwa na Katibu Tawala wa Mkoa, Mh. Jacob.

Wakati huohuo, kwenye nafasi ya Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha, Mhe. Maximilian Iranghe alipigiwa kura 34, ambapo 33 zilikuwa za ndiyo na kura 1 ikiwa ya hapana.

Sauti ya Naibu Meya na Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha wakila kiapo

Akizungumza baada ya zoezi hilo, Mkuu wa wilaya ya Arusha, Modest Joseph Mkude, aliwapongeza madiwani waliokula kiapo na kuwataka kuzingatia maadili, kushirikiana katika utekelezaji wa majukumu, na kufuata sheria za nchi wakati wote wa utumishi wao.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Arusha, Modest Joseph Mkude