Savvy FM

NIDA, Leseni au Pasi ya Kusafiria kutumika kupigia kura

October 19, 2025, 11:10 pm

Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Arusha Mjini akiwa kwenye mkutano, Shabani Ferdinand Manyamba.Picha na Jenipha Lazaro

Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Arusha Mjini, Shabani Ferdinand Manyamba, ametangaza rasmi kuwa Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani utafanyika siku ya Jumatano, tarehe 29 Oktoba 2025, kwa mujibu wa Kifungu cha 69(1) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya mwaka 2024.

Na Jenipha Lazaro

Akizungumza katika ukumbi wa Jiji la Arusha, Bw. Manyamba amesema kuwa kwa mujibu wa tangazo hilo, vituo vilivyotumika kuandikisha wapiga kura ndivyo vitakavyotumika kupigia kura siku ya uchaguzi.

Sauti ya Shabani Ferdinand,Msimamizi wa Jimbo la Arusha Mjini

Sambamba na hayo, mawakala kutoka vyama vya NLD na CUF wamesema kuwa wanaendelea na kampeni, lakini wanakabiliwa na ukata wa fedha hali ambayo inawakwamisha kuwafikia wananchi kwa wakati.

Sauti ya kiongozi wa CUF akielezea changamoto ya fedha kwenye kampeni

Naye kiongozi wa NLD ameelezea kilio chake juu ya ukata huo

Sauti ya kada wa NLD akielezea changamoto za kampeni