Savvy FM
Savvy FM
October 18, 2025, 10:15 pm

Kufuatia kikao cha mkutano mkuu wa Kijiji cha Nambere kata ya sokoni 2 hapa mkoani Arusha kilichofanyika mwanzoni mwa mwezi huu, wananchi wa kijiji hicho wameazimia kuchukua hatua kali dhidi ya mmomonyoko wa maadili kwa vijana, kina mama pamoja na wazee, hatua iliyowapelekea kuunda kamati ndogo ya maadili na nidhamu.
Na Jenipha Lazaro
Katibu wa Kamati ya Maadili, Evarest Mbalakai, amewataka viongozi wa makundi yote kuhakikisha wanasimamia maazimio ya kikao hicho kwa uaminifu ili kufanikisha lengo kuu la kurejesha maadili kwenye jamii ya Nambere.
Kwa upande wake, mmoja wa wananchi wa kijiji hicho, Neema Laizer, amepongeza juhudi hizo na kusema kuwa jamii iko tayari kushirikiana na viongozi wa dini na wazee kutekeleza maazimio hayo bila kubagua jinsia.