Savvy FM
Savvy FM
October 13, 2025, 10:42 pm

Kuelekea maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere, jumuiya za wazee wa mkoa wa Arusha wameandaa matembezi ya amani ikiwa na lengo la kumuenzi.
Na Jenipha Lazaro
Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Umoja wa Wazee Mkoa wa Arusha Munga Emanuel amesema matembezi haya yataambatana na uchunguzi wa afya kwa wazee, upimaji wa macho na utoaji wa miwani bure pamoja na kusema lengo ni kuendelea kutambua mchango wa Hayati Baba wa Taifa ambaye ni muasisi wa amani, umoja na mshikamano wa taifa, ambayo matembezi hayo yataenzi kazi na falsafa zake zilizotoa mchango mkubwa katika kujenga ujenzi na ustawi.
Aidha kwa upande mwingine, mwenyekiti huyo amesema matembezi hayo yataanzia eneo la Makumbusho na kumalizika Mnara wa Mwenge.
Mgeni rasmi wa matembezi haya anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha huku kauli mbiu ikibebwa na Amani, Kazi, Utu, Umoja na Mshikamano wa Taifa.