Savvy FM
Savvy FM
October 13, 2025, 10:27 pm

Zikiwa zimesalia siku chache kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani, mamia ya wananchi wa Kata ya Ungalimitedi wamejitokeza kwa wingi katika Mtaa wa Darajani kumsikiliza mgombea udiwani wa Kata ya Ungalimited kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Mahamoud Said Omary, ambaye ameendelea na kampeni zake za kuomba ridhaa ya kuiongoza Kata hiyo kwa kipindi kingine cha miaka mitano.
Na Jenipha Lazaro
Akizungumza katika mkutano huo wa kampeni, Mahamoud Said Omary ameeleza mafanikio mbalimbali aliyoyapata wakati wa uongozi wake wa miaka mitano iliyopita, yakiwemo;Ujenzi wa shule ya sekondari ya Kata,ujenzi wa vivuko kwa ajili ya kurahisisha usafiri wa wananchi,ushirikiano na wadau mbalimbali uliowezesha upatikanaji wa madawati zaidi ya 300 katika shule zote ndani ya kata hiyo.
Ameahidi kuwa, endapo atachaguliwa kwa kipindi kingine, atahakikisha ujenzi wa shule ya msingi ya Ungalimited yenye madarasa ya ghorofa ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi na kupunguza msongamano.
Kwa upande wao, baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo wamesema