Savvy FM

Serikali yawainua wananchi kiuchumi kupitia mradi wa TASAF

September 23, 2025, 1:01 pm

Mkuu wa wilaya ya Arusha Mhe. Joseph Modest Mkude.Picha na Jenipha Lazaro

Mkuu wa wilaya ya Arusha Mhe. Joseph Modest Mkude amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita imeendelea kuwainua watu kiuchumi kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo mradi wa TASAF, ambapo takribani walengwa 4,877 wamenufaika na mradi huo jijini Arusha kwa fedha zaidi ya bilioni tatu zilizotolewa katika ipatayo miradi 35.

Na Jenipha Lazaro

Ameyasema hayo wakati alipokutana na waandishi wa habari jijini Arusha na kuongeza kuwa, halmashauri zote nchini zimeendelea kusisitizwa kutoa asilimia 10 za mapato kwa ajili ya mikopo kwa makundi maalumu ambapo zaidi ya bilioni 10 zimetengwa na vikundi 853 vimenufaika, huku zaidi ya bilioni 11 zikitengwa mwaka huu kwa ajili ya kutolewa kwa makundi hayo maalumu.

Sauti ya Joseph Modest Mkude,Mkuu wa Wilaya ya Arusha

Kwa upande mwingine Mkude amewataka dereva bodaboda kuendelea kufuata Sheria za barabarani

Sauti ya Joseph Modest Mkude,Mkuu wa Wilaya ya Arusha