Savvy FM
Savvy FM
September 1, 2025, 3:48 pm

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Amos Makalla, ameanza rasmi ziara yake ya kikazi mkoani hapa kwa kutembelea taasisi mbalimbali za kidini, akianza na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) ambapo ametoa wito kwa viongozi wa dini kuendelea kushirikiana na serikali katika kuleta maendeleo kwa wananchi.
Na Jenipha Lazaro
Akizungumza katika Ofisi za BAKWATA zilizopo katika msikiti mkuu wa Ijumaa, Bondeni, RC Makalla amesema kuwa serikali inatambua na kuthamini nafasi ya viongozi wa dini katika jamii, hasa katika kipindi hiki ambapo nchi inaelekea kwenye uchaguzi.
Naye Sheikh wa Mkoa wa Arusha, Sheikh Shaban Abdala, alimhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa viongozi wa dini wataendelea kuwa wadau wakuu wa maendeleo katika kila awamu ya uongozi wa serikali
Kwa upande wake, Katibu wa BAKWATA Mkoa wa Arusha, ndg. Ali Nassor, alieleza kuwa taasisi hiyo imejipanga kutumia maadhimisho ya sikukuu ya Maulid kama jukwaa la kuhubiri na kutangaza amani, hasa kipindi hiki cha uchaguzi, kwa kushirikiana na serikali