Savvy FM
Savvy FM
May 26, 2025, 12:58 pm

Mgogoro wa barabara uliodumu kwa takribani wiki mbili baina ya wananchi na mwekazaji katika kata ya Olmot mtaa wa Mateves Ngaramtoni ya chini umetatuliwa na wananchi kupata barabara.
Na Gasper Sambweti
Wakizungumza na Savvy FM wananchi wa Ngaramtoni ya chini wamemshukuru Mwenyekiti wao ndugu Ibrahim Urasa , ambae kwa kushirikiana na uongozi wa mtaa na mbunge wa jimbo la Arusha mjini Mhe. Mashaka Mrisho Gambo ambae alitembelea eneo la mgogoro na kuushauri uongozi wa mtaa huo kuwasiliana na mwekazaji ambae alidaiwa kutaka kufunga barabara hiyo.
Kwa upande wake balozi wa mtaa wa Mateves ndugu Rafael Rishati Mollel ameelezea jinsi walijitolea kutoa hatua mbili na nusu za shamba lake na mwekezaji nae kutoa hatua mbili na nusu ili kupatikana kwa mita 5 za barabara hiyo.
Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Ngaramtoni ya chini bwana Ibrahim Urasa ameshukuru wananchi na viongozi pamoja na mwekezaji kwa maridhiano hayo ya kuleta maendeleo katika mtaa wa Ngaramtoni ya chini.