Savvy FM
Savvy FM
May 6, 2025, 2:00 pm

Taharuki imetokea baada ya mwili wa marehemu kurudishwa mochwari mara mbili kabla ya kuzikwa.
Na Michael Nanyaro
Kundi la vijana wa bodaboda maarufu kama wadudu wilayani Arumeru jijini Arusha wamemrudisha mwenzao aliyefariki mochwari baada ya mwili kufikishwa nyumbani na familia, na vijana hao kusema familia haikufuata taratibu za ‘wadudu’.
Wakizungumza baadhi ya vijana hao wamesema sababu za mwili wa marehemu kufikishwa nyumbani na familia na wao kuuchukua na kuupeleka mochwari zinatokana na familia ya marehemu Benson Isack maarufu Urassa kuuchukua mwili huo mapema saa kumi na moja alfajiri wakati taratibu za wadudu mwili kuchukuliwa ni saa nne asubuhi.
Naye dereva wa gari maalumu la kubebea mauti Fikiri Brayan amesema wanafamilia walikubalina mwili utoke mochwari saa 12 asubuhi lakini baada yakurudi walipofika maeneo ya nyumbani walizuiliwa na marafiki wa marehemu.
Kwa upande wa diwani wa kata ya Mbureni Faraja Maliaki amesema kitendo hicho ni fedhea kwa wananchi na familia ya marehemu na kuwataka vijana kutubu na kumrudia Mungu.
Hata hivyo mwili wa marehemu umezikwa tayari hapo jana jioni baada ya marafiki na familia kukubaliana kwa pamoja ratiba ya maziko ya mpendwa wao.