Savvy FM

Changamoto za Bonde la mto Nduruma fursa kwa wananchi

May 2, 2025, 1:06 pm

Pichani ni bonde la mto Nduruma likiwa limejaa maji kutokana na mvua- Picha na Jenifa Lazaro

Takribani wananchi elfu kumi katika Kata ya Mbuguni Wilayani Arumeru Mkoani Arusha waliokuwa wakipata athari mbalimbali ikiwemo kupoteza makazi na maisha ya watu kutokana na bonde la Mto Nduruma kujaa maji wameanza kupata ahueni baada ya bonde hilo kudabuliwa.

Na Jenifa Lazaro

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara katika mto Nduruma Segule Segule Mkurugenzi wa Bodi ya maji Bonde la Pangani amesema utekelezaji wa mradi wa udabuaji wa bonde la Mto Nduruma ni endelevu ili kuondoa maji yasiweze kuleta athari kwenye maisha ya watu.

Sauti ya mkurugenzi wa bodi ya maji Bonde la Pangani, Segule Segule

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Rasilimali Maji kutoka Wizara ya maji Rosemary Rebugisa amesema umuhimu wa udabuaji wa bonde hilo Wizara ya maji kupitia idara hiyo imeweka kipaumbele katika kufanya uhifadhi wa vyanzo vya maji na kujenga mabwawa kwa ajili ya kuhakikisha maji yanayo hifadhiwa yanavunwa na kusaidia jamii katika kuboresha maisha.

Sauti ya Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Rasilimali Maji kutoka Wizara ya Maji Rosemary Rebugisa 

Nao baadhi ya wananchi wa Kata hiyo ya Mbuguni wamewashukuru bonde la Pangani kwakuweza kutatua changamoto hiyo.

Sauti ya mwananchi

Bodi ya bonde la Pangani inaendelea na zoezi la udabuaji ( kuongeza kina na upana ) wa mto Nduruma ili kukabiliana na athari za mafuriko kwenye makazi ya watu na mashamba yao.