Radio Kwizera

Akamatwa akiomba Rushwa ya ngono

April 9, 2021, 12:33 pm

Na; Anord Kailembo

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoani Kagera inamshikilia mkufunzi wa chuo cha kilimo Maruku kwenye Manispaa ya Bukoba kwa tuhuma za Rushwa ya Ngono

Mkuu wa Takukuru mkoani Kagera Bw John Joseph amemtaja mkufunzi huyo kuwa ni Ruta Kyarangaine mwenye umri wa miaka 59

Mkuu wa Takukuru Kagera Bw John Joseph akizungumzia tukio hilo

Amesema baada ya TAKUKURU kupata taarifa April 3 mwaka huu iliweka mtego ambapo maafisa wa TAKUKURU walimkamata mkufunzi huyo kwenye nyumba ya wageni mjini Bukoba akiwa na mwanafunzi huyo akilazimisha kupewa Rushwa ya ngono

Sauti ya Mkuu wa Takukuru

Aidha amesema kuanza kuripotiwa kwa vitendo hivyo ni matokeo ya kampeni iliyoanzishwa mwaka jana ya kutoa elimu ya namna ya kukabiliana na vitendo vya Rushwa ikiwemo Rushwa ya ngono