Mtegani FM

Jamii yatakiwa kuacha mfumo dume, iruhusu wanawake kusikiliza redio jamii

30 November 2024, 12:14 pm

Wananchi Wa Kijiji Cha kizimkazi Mkunguni Watakiwa Kuacha Mila Potofu Za Kutowaruhusu Wanawake Kutumia Radio Jamii.

Na Mwaka Mohd Mwita.

Hayo yamesemwa na Ustadh Yahya katika kijiji cha Kizimkazi Mkunguni wakati akiongea na Mtegani FM radio. Amesema kuwa jamii sasa inatakiwa kuacha kuwakandamiza wanawake kwa kutosikiliza radio jamii badala yake waamke na kuwaruhusu wanawake kusikiliza radio jamii ili ziweze kuwaletea mabadiliko na maendeleo.

Ameongezea kusema kuwa mwanamke kusikiliza radio siyo jambo jipya au linaweza kwenda kinyume na maadili ya dini ya kiislamu, hivyo jamii inatakiwa iwape wanawake uhuru wa kusikiliza radio jamii.

Sauti ya Ustadh Yahya.

Kwa upande wao wanawake wa kijiji cha Kizimkazi wamewataka wanawake wenzao kusikiliza radio jamii kwani zina mchango mkubwa sana katika maisha yao.