Mtegani FM
Mtegani FM
14 July 2025, 5:52 pm

Mkuu wa Mkoa Kusini Unguja ameahidi makubwa kufuatia uteuzi wake pamoja na utambulisho wake uliofanyika katika ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja.
Na Miraji Manzi Kae
Hayo ameyasema leo 14 Julai 2025 katika ofisi za Mkuu wa Wilaya Kusini Unguja Makunduchi ambapo ameahidi kufanya kazi kwa kuzingatia weledi na kuahidi kufanya kila jambo kwa ajili ya wananchi wote waliokuwa na changamoto zao,
Ameongeza kwa kusema kuwa anahitaji kupewa ushirikiano wa kitosha kama walivyowahi kupewa wakuu wa mikoa waliopita, kwani kupewa kwake ushirikiano ndiko kutakakoweza kufanya kazi kwa bidii na kwa ufanisi mkubwa. Ameongeza kuwa anahitaji ushirikiano mkubwa na wananchi wa Kusini, ukizingatia yeye ni Mkuu wa Mkoa wa kwanza mwanamke hii inaenda kuleta mwanga pia kuona wanawake wanapata fursa katika ngazi za uongozi.
Kwa upande wao wananchi wa Mkoa wa Kusini wameahidi kuwa naye bega kwa bega katika kumpa ushirikiano ili kufanikisha kazi yake ya utumishi katika mkoa wao.