Mtegani FM

Kituo cha kujifunza lugha ya alama chaleta mwanga kwa viziwi

12 July 2025, 4:30 pm

Picha ikionesha meza kuu ya viongozi mbali mbali waliohudhuria katika shuhuli ya mahafali ya 6 ya chuo cha INCLUSIVE VOCATIONAL TRAINING CENTER (IVTC) Na alieshika mike ni mgeni rasmi ndugu mustafa mohd haji, Picha na Miraji manzi kae

Wanafunzi waliohitimu chuo cha kujifunza lugha ya alama kijulikanacho kama Inclusive Vocational Training Center (IVTC) watakiwa kutumia mafunzo yao ya uhitimu kuleta nuru na mwanga kwa watu wote wenye ulemavu wa uziwi.

Na Miraji Manzi Kae

Hayo Yamesemwa Katika Ukumbi wa mitihani skuli ya Kizimkazi Dimbani, katika mahafali ya 6 ya chuo cha kujifunza lugha ya alama kijulikanacho kama inclusive vocational training center (IVTC) Ambapo wahitimu wa mafunzo hayo wametakiwa, kutumia mafunzo hayo kuwa chachu ya kuwaelimisha watu wenye ulemavu wa uskivu, na kuwacha kuwaona watu wenye ulemavu wa uskivu kama kero , na badala yake kutambua nao wana haki kama watu wengine.

Picha ikimuonesha mkufunzi wa Chuo Cha (IVTC)

Ameongezea kusema kuwa watu wenye ulemavu wa uskivu pia wana haki ya kwenda kujiandikisha katika daftari la kupiga kura na kuchagua viongozi pia.

Sauti Ya Mkuu Wa Kituo Cha (IVTC)

Nae mgeni rasmi ndugu mustafa mohd haji amesema serikali ya wilaya kwa kutambua uwepo wa watu wenye uskivu, umetoa fursa ya kuwapatia fedha watu wenye ulemavu wa uskivu kwa ajili ya kufanyia ujasiriamali na fedha hizo wameanza kuzitoa kwa watu aina hiyo bila ya riba.

Sauti Ya Mgeni Rasmi Ndugu Mustafa Moh’d Haji.

Kwa Upande wao wahitimu wa mafunzo hayo wameahidi kutumia mafunzo hayo vizuri kwa ajili ya kutoa faraja kwa watu wenye changamoto hiyo ya uskivu, na kutoa risala fupi kuhusu malengo ya chuo hicho na kuanzishwa kwake.

Sauti Ya Mwanafunzi Alietoa Risala Fupi Ya Chuo Cha (IVTC).