Mtegani FM

Wanakijiji Wa Kajengwa Wawatolea Uvivu Viongozi Wa Hoteli Ya Reef

28 June 2025, 2:35 pm

Picha ikionesha wanakijiji wa kajengwa makunduchi wakiwa katika kikao na mkuu wa wilaya ( picha na Miraji Manzi Kae )

Wanakijiji Na Wajasiriamali Wa Kijiji Cha Kajengwa wameulalamikia uongozi wa hoteli ya reef beach kwa kuwazuilia kutokufanya biashara zao na kupita katika eneo la fukwe liliopo mbele ya hoteli hiyo ambayo nikinyume na taratibu.

Na Miraji Manzi

Wakitoa malalamiko hayo mbele ya mkuu wa wilaya ya kusini wajasiriamali hao wamesema kua kitendo cha kuzuiliwa kulitumia eneo hilo kwa shughuli yoyote ikiwemo biashara zao limewavunja moyo ikiwa wao tayari wamejiajiri kupitia sekta hiyo ya utalii. 

Wamesema kua mbali ya kuzuiliwa kwao kwa biashara zao lakini pia wanahofia usalamaa wao pamoja na biashara zao kutokana na walinzi wa hoteli hiyo kuwatishia amani pindi wanapotumia ufukwe huo.

Mkuu Wa Wilaya Mh. Othman Ali maulidi Amewaomba Wanakijiji Hao kufuata taratibu zilizowekwa na serekali ikiwemo kutokuwafata wageni katika makazi yao na badala yake wawe na maeneo maalum Watakayoyatumia kwa biashara zao.