Kagera Community Radio

Jamii Kagera yaaswa kuacha uchomaji mbuga hovyo

August 19, 2025, 3:20 pm

Moto ukiwaka mbugani

Baadhi ya wananchi mkoani Kagera wameaswa kuachana na vitendo ya uchomaji hovyo mbuga na mistu ili kutunza mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Na Anold Deogratias

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kagera limetoa onyo kali kwa wananchi wanaochoma hovyo mbuga na kwamba wakibainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao ikiwemo kufikishwa mahakamani.

Rai hiyo imetolewa na Kamanda wa jeshi hilo mkoa wa Kagera Joseph Ngonyani wakati akizungumza na vyombo vya habari, ambapo ameeleza kuwa uchomaji wa mbuga licha ya kupunguza mvua lakini pia moto huo unaweza kusababisha madhara ikiwemo kuunguza makazi ya watu.

Sauti ya Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kagera Joseph Ngonyani

Aidha kamanda Ngonyani amewataka wananchi na viongozi kuendelea kutoa taarifa juu ya wale ambao wamekuwa wakijiusisha na vitendo vya uchomaji hovyo mbuga na mistu ili kuweza kudhibiti vitendo hivyo katika mkoa wa Kagera.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kagera Joseph Ngonyani

Kamanda Ngonyani amewataka wananchi kutoa taarifa kwa jeshi ili wakati wanataka kuchoma vitu kama takataka waweze kusaidia kudhibiti moto endapo utakuwa mkali lakini pia ameiasa jamii kutoa taarifa kwa jeshi hilo kwa kupiga simu bure namba 114 pindi wanapoona tukio la moto mkali.

Sauti ya kamanda Joseph Ngonyani

Baadhi ya jamii mkoani Kagera hasa wakulima na wafugaji wamekuwa na tabia ya uchomaji mashamba wakati wa maandalizi ya kilimo, huku wafugaji wakichoma mbuga kwa ajili ya malisho mapya ya mifugo.