Kagera Community Radio
Kagera Community Radio
May 8, 2025, 1:03 pm

Na Mwandishi wetu
Madaktari Bingwa na Bingwa Bobezi wa Rais Samia wamehitimisha kambi ya utoaji huduma za kibingwa katika halmashauri zote nane (8) za mkoa wa Kagera ambapo wananchi wameomba utaratibu huo kurasimishwa ili waendelee kuwapunguziwa gharama za matibabu.
Wakihojiwa na Mwandishi wa Kagera Community Radio baadhi ya wananchi waliojitokeza kupata huduma wameomba kambi hizi za madktari bingwa ziiingiwe katika mpango wa wizara ili ziwe rasmi kwa kila hospitali nchini badala ya kufanyika mara moja au mbili kwa mwaka.
DR Mwombeki John kutoka Wizara ya Afya anayeratibu zoezi hilo akihojiwa na mwandishi wa Kagera Community Radio juu ya huduma hityo amesema mkoa wa Kagera umekuwa ukitumia gharama kubwa kwa ajili ya rufaa za wagonjwa kuelekea hospitali kubwa za Bugando na Chato lakini uwepo wa madaktari hao katika hospitali za mkoa na wilaya umeleta nafuu kubwa ya gharama za matibabu ya huduma za kibingwa.
Aidha Mkuu wa wilaya ya Bukoba Ernest Siima amesema kuwa pamoja na changamoto zilizopo, mkoa wa Kagera umeendelea kuboresha huduma za Afya ya Uzazi na Watoto akibainisha kuwa takribani asilimia 90 ya akina mama wamehudumiwa katika vituo vya kutolea huduma kwa mwaka 2024.
Amezitaja changamoto zilizopo katika huduma ya Afya ya Uzazi na Watoto kuwa ni upungufu wa watumiushi wenye ujuzi, upungufu wa vifaa tiba, magari ya kubebea wagonjwa wanaohitaji rufaa, miundombinu ya barabara na upungufu wa damu salama.
Huduma za kibingwa amazo zimetolewa ni pamoja na huduma za ubobezi wa watoto wachanga, magonjwa ya wanawake na ukunga, upasuaji bobezi wa mfumo wa mkojo, ubingwa wa usingizi na ganzi, magonjwa ya ndani, meno na wauguzi wakunga wabobezi.