Kagera Community Radio

Wananchi Bukoba watakiwa kujielimisha kuhusu migogoro ya ardhi

April 23, 2025, 11:57 am

Baadhi ya wananchi wakipata elimu ya migogoro ya ardhi shambani.

Ardhi inavyoweza kuwa chanzo cha kuondoa umaskini badala ya kusababisha migogoro katika jamii.

Na Shemsa Musa

Wananchi manispaa ya bukoba wametakiwa kujielimisha kwa lengo la kuwa na ufahamu juu ya masuala mbali mbai ya ardhi kwa lengo la kupunguza migogoro.

Akizungumza na kcr fm mtaalam wa upimaji kutoka ofisi ya ardhi mkoa wa kagera bwana Leonidas Patrik amesema watu wengi wamekua wakisababisha migogro kwa kutojua na wengine wakidhani wanafahamu masuala hayo kumbe sio kweli.

Aidha bwana Patrik amesema kuna baadhi ya watu amao wamekua wakitafsiri vibaya sharia ya ardhi jambo ambalo pia limekua likipelekea migogoro hiyo.

Sauti ya Bw Patrick Leonard mtaalamu wa upimaji ardhi mkoani Kagera