Bunda FM Radio
Bunda FM Radio
September 12, 2025, 7:14 pm

“Tuna malengo ya kufanya vizuri msimu ujao na kushika nafasi ya nne za juu ili tupate nafasi ya kucheza ngao ya jamii’’ Kocha mkuu wa Bunda queens Aley Ibrahimu
Na Amos Marwa
Timu ya soka ya wanawake Bunda Queens inayoshiriki ligi kuu ya wanawake Tanzania bara imeendelea na mandalizi ya msimu mpya kwa kufanya mazoezi katika uwanja wa shule ya msingi Miembeni wilayani Bunda.
Akizungumza na Bunda FM , Baada ya maozoezi ya asubuhi uwanjani hapo kocha mkuu wa timu hiyo Aley ibrahimu amesema maandalizi yanaendelea vizuri na anaamini vijana wake watafanya vizuri katika msimu mpya wa 2025/2026.
Aidha, ameongeza kuwa wameondokewa na wachezaji wake watatu akiwemo Ester Maseke alietimkia Jkt quuens waliokuwa tegemeo katika kikosi hicho lakini timu hiyo imesajili wacheza wa kuchukua nafasi zao na watafanya vizuri, kwani wamesajili wachezaji bora na kupandisha wachezaji wengine kutoka timu ya vijana.
Kwa upande wake nahodha wa timu hiyo Jamila Celestine kwa niaba ya wachezaji wenzake amesema wamejiandaa vizuri kukabiliana na mikikimikiki ya ligi hiyo na kuwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi katika michezo yao kwa ajili ya kuwapa hamasa.
Msimu uliyopita timu ya Bunda queens ilimaliza ligi katika nafasi ya 6 ikiwa imejikusanyia jumla ya alama 19 baada ya kushuka dimbani michezo 16 wakishinda michezo 5 wakisare michezo 4 na kupoteza michezo 7.
