Bunda FM Radio
Bunda FM Radio
May 21, 2025, 11:50 am

”Madiwani shirikianeni na watendaji wa mitaa pamoja na wazazi ili kuhakikisha upatikanaji wa chakula cha mchana kwa ajili ya wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari”, Salum K. Mtelela katibu tawala Wilaya ya Bunda.
Na Amos Marwa
Katibu tawala wa wilaya ya Bunda Salum Alfan Mtelela amewataka Madiwani washirikiane na wakuu wa idara ya elimu kuhakikisha upatikanaji wa Chakula mashuleni ili kuongeza ufaulu kwa Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.
Akiwasilisha salamu za Serikali katika Baraza la Madiwani lilofanyika kwenye Ukumbi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Mtelela amesema wilaya ya Bunda ni moja ya wilaya zinazofanya vizuri katika suala la chakula mashuleni na inapaswa kuongeze nguvu katika suala hilo.
Aidha katibu tawala amesema kuwa pamoja na jitihada za serikali kuimarisha miondombinu katika mashule pia ameongeza kuwa suala la madili kwa wanafunzi ni la kutiliwa mkazo ili kuondoa nidhamu mbovu kwa wanafunzi ikiwemo matumizi ya Simu mashuleni na vitendo vya mapenzi ya jinsi moja.
Kwa upande mwingine baraza la madiwani la Halmashauri ya Mji wa Bunda limejadili kuhusu Malipo ya Posho kwa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, ujenzi wa Soko la Bunda mjini, ujenzi wa Zahanati mbalimbali na changamoto za upatikanaji wa maji kwa Wananchi katika halmashauri ya Mji wa Bunda.
