Buha FM Radio

Kabanga kuendesha kambi ya madaktari bingwa

6 Aprili 2026, 09:51

Baadhi ya madaktari wa hospitali ya rufaa Kabanga wakiwa katika mazungumzo ya pamoja kuelekea kambi ya madaktari bingwa. Picha na Sharifat Shinji.

Wananchi wilayani Kasulu na mkoa wa Kigoma kwa ujumla waombwa kujitokeza siku ya kambi ya madaktari bingwa katika hospitali hiyo.

Na; Sharifat Shinji

Hospitali ya Rufaa Kabanga wilayani Kasulu mkoani Kigoma inatarajia kuwa na Kambi ya madaktari bingwa kuanzia tarehe 13 hadi 17 mwezi April, 2026 kwa lengo la kuwasaidia wakazi wa Mkoa wa Kigoma na maeneo jirani wenye changamoto mbalimbali za kiafya.

Hayo ameyasema Afisa mahusiano wa hospitali hiyo Bi. Neema Mwaipopo wakati akizungumza kwa niaba ya Mganga mfawidhi wa Hospitali Dkt. Peter Kitenyi, ambapo amesema kambi hiyo itawezesha utoaji wa huduma mbalimbali za kibigwa kwa wananchi wote wa Wilaya ya Kasulu na maeneo jirani.

Sauti ya Mwaipopo.

Aidha Mwaipopo amesema hospitali inapokea na kutoa huduma kwa wagonjwa wote wenye bima na wasio na bima huku akiwakaribisha wananchi waote wa Wilaya ya Kasulu kujitokea kupata huduma za kibingwa katika hospitali hiyo.

Sauti ya Mwaipopo.
Afisa Uhusiano hospitali ya rufaa Kabanga Bi. Neema Mwaipopo. Picha na Sharifat Shinji.

Hospitali ya Rufaa Kabanga huwa inaandaa Kambi ya madaktari Bingwa kila mwezi kwa lengo la kuwahudumia wananchi wenye changamoto mbalimbali za matibabu ya kibingwa, kambi hiyo huandaliwa na hospitali ya Kabanga kwa kushirikiana na madakitari bingwa kutoka hospitali ya rufaa Kabanga.