Buha FM Radio
Buha FM Radio
10/03/2026, 22:02

“Wakulia wakitumia mkojo wa sungura kama tiba mbadala ya kuua wadudu itawasaidia kupuguza gharama za manunuzi ya kemikali na madawa kwa ajili ya kua wadudu wanaoshambulia mazao” Amesema Chiza.
Na; Helbeth Barayata
Wakulima wa mboga mboga katika Halmashauri ya Miji Kasulu Mkoani Kigoma wameshauriwa kutumia njia mbadala katika urutubishaji na matumizi ya viuatirifu kwa kutumia mkojo wa sungura.
Akizungumza na Buha FM radio Mema Chiza ambaye ni mfugaji na mkulima msomi na mzoefu katika Nyanja hizo, amesema matumizi sahihi ya mkojo wa sungura kwa kuchanganya sabuni na maji hutumika kama viuatirifu kisicho na kemikali hivyo kupunguza gharama za uendeshaji wa kilimo hicho.
Aidha amebainisha kuwa ufugaji wa sungura unambatana na faida nyingi huku akitoa wito kwa wakulima kutumia njia za asili kwa usahihi katika kilimo cha mboga, matunda na mazao mengine ili kupunguza matumizi ya kemikali.

Hata hivyo amehitimisha kwa kusema kuwa mkojo wa sungura umekuwa na upekee kutokana na kiwango sahihi cha ammonia kinachopatikana katika mkojo huo.