Buha FM Radio
Buha FM Radio
05/03/2026, 17:21

“Ufugaji wa nyuki una faida nyingi kutokana na matumi zake kuwa mengi pia”
Na; Helbeth Barayata
Wananchi wa Halimashauri ya Mji kasulu mkoani Kigoma wameshauriwa kujishughurisha na ufugaji wa nyuki, uchakataji na uuzaji wa mazao yanayotokana na mazao ya asali ili kujiongezea kipato pamoja kuinua uchumi wa nchi.
Akizungumza na Buha fm Radio Ndg. Staford Nkubhagana ambaye ni mfugaji wa nyuki, mchakataji wa asali, muuzaji wa asali na mkurugenzi wa kampuni ya NAFCO kupitia kipindi cha Darasa nje ya shule amesema uhitaji wa asali na bidhaa zitokanazo na asali katika mkoa huo ni mkubwa huku wazalishaji akitaja kuwa wachache.
Aidha amebainisha kuwa wazalishaji wanatakiwa kujikita na ufugaji wa kisasa wenye tija ambao unazingatia ubora wa masoko ya kitaifa na kimataifa, na kuwaomba wadau kuhudhuria mafunzo mbalimbali yanayohusu ufugaji wa nyuki ili kukuza uzalishaji wa zao hilo.

Katika hatua nyingine Nkubhagana amesema ufugaji wa nyuki kwa njia ya kisasa una faida kubwa kwakua kupitia asali kuna bidhaa nyingine saba hupatikana ikiwa ni pamoja na inta, mkate wa watoto wa nyuki, sumu ya nyuki, mafuta ya ngozi, waini, na bidhaa nyingine zinzotokana na zao hilo.
Hata hivyo ameshauri wafugaji kujikita katika uzalishaji wa mazao ya asali ili kupata uzoefu katika eneo hilo, na mara baada ya kupata ujuzi zaidi wajihusishe na uchakataji wa bidhaa nyingine zinazotokana na mazao ya nyuki.