Madiwani watwishwa zigo kuzuia upotevu wa mapato Kasulu
Buha FM Radio

Madiwani watwishwa zigo kuzuia upotevu wa mapato Kasulu

February 5, 2026, 10:11 pm

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kasulu na diwani wa kata ya Kigondo Ayubu Ngalaba akizungumza mbele ya Balaza la Madiwani. Picha na Ramadhan Zaidy.

Baada ya Madiwani wa Halmashauri ya Mji Kasulu kupitisha bilioni 43 kama bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027 wameagizwa kusimamia mianya yote inayosababisha kupotea kwa mapato katika Halmashauri hiyo.

Na; Ramadhan Zaidy

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kasulu na diwani wa kata ya Kigondo Ayubu Ngalaba amewataka
mdiwani ndani ya Halmashauri hiyo kuzuia mianya ya upotevu wa mapato ili kuhakikisha wanafikia lengo la bajeti iliyopitishwa.
Akizungumza katika Kikao cha Baraza la madiwani wa Halmashauri hiyo Ngalaba amesema ushiriki
wa moja kwa moja wa madiwani hao utasaidia kurahisisha shughuli ya ukusanji wa mapato ndani ya kata wanazoziongoza.

Sauti ya Mwenyekiti Ayubu Ngalaba.

Aidha Mkuruganzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu Mwl; Vumilia Simbeye amesema Halmashauri itafanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa na baraza hilo ili kuhakikisha miradi yote iliyopangwa inatekelezwa.

Sauti ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu Mwl. Vumilia Simbeye.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu Mwl. Vumilia Simbeye. Picha na Ramadhan Zaidy.

Akiwasilisha salamu za Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Katibu Tawala wa Wilaya hiyo
Bi; Theresia Mtewele amewasihi madiwani kutoa elimu kwa wananchi wao juu ya kuchangamkia fursa
na kuanza kulima mazao ya kimkakati.

Sauti ya Katibu Tawala wa Wilaya Kasulu Bi; Theresia Mtewele.
Katibu Tawala wa Wilaya Kasulu Bi; Theresia Mtewele akiwasilisha salamu za Mkuu wa Wilaya hiyo. Picha na Ramadhan Zaidy.

Nao baadhi ya wajumbe walioshiriki katika kikao hicho wamesema utekeleza mzuri wa bajeti hiyo ndiyo
misingi ya maendeleo ya Halmashuri hiyo wakisisitiza madiwani kuwajibika kikamilifu ili kufikia malengo.

Sauti za wajumbe walioshirikia kikao hicho.

Baraza la madiwani katika Halmashauri ya Mji Kasulu limepitisha na kuinisha Bajeti ya zaidi ya
Shilingi Bilioni 43 kwa mwaka wa fedha wa 2026/2027 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Halmashauri hiyo.

Baadhi ya Madiwani wakiwa katika Baraza la Madiwani. Picha na Ramadhan Zaidy.