Buha FM Radio
Buha FM Radio
January 31, 2026, 2:46 pm

Halmashauri ya Mji Kasulu imejipanga kukusanya zaidi ya bilioni 40 katika mwaka wa fedha 2026/2027 ikiwa ni ongezeko la asilimia 14 kutoka bajeti ya mwaka 2025/2026.
Na; Irene Charles
Kaimu mkurugenzi wa Hmji Kasulu Ndg. Nurfus Aziz amesema katika mwaka wa fedha 2025/2026 mapato ya nusu mwaka katika halmashauri hiyo walifanikiwa kukusanya shilingi bilioni 1.7.
Amesema hayo wakati wa kikao cha ushauri wa bajeti (DCC ) na kusema licha ya kupata fedha hizo bado kumekuwepo na changamoto ikiwa ni pamoja na utegemezi wa bajeti na kuchelewa kupokelewa kwa fedha za maendeleo.
Aidha ndg. Nurfus amesema wameandaa mikakati inayoweza kufanikisha kufikia malengo, kwa kuimalisha mapato ya ndani kupitia vyanzo mbalimbali ikiwa ni vya unenepeshaji wa mifugo, kupima magari kwenye mzani eneo soko la mnadani na kukodisha maeneo.

Mbali na hayo Kaimu mkurugenzi Nurfus Aziz amesema wataendelea kuzungumza na wananchi kuwasaidia kuwachangia shughuli za miradi ya maendeleo na kutenga nafasi za ajira ili kupata idadi ya watumishi walipo katika Halmashauri huku akieleza makisio na bajeti kwa mwaka wa fedha 2026/2027 ndg. Nurfus amesema halmashauri inatarajia kukusanya shilingi bilioni 43 kupitia vyanzo vyote vya halmashauri ikiwa ni ongezeko la asilimia 14.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Halmashauri Kasulu na mwenyekiti wa kamati ya halmashauri (DCC) Kanali Isacck Mwakisu amesema kwa sasa kitu kinachofanya halmashauri kutovuka na kuingia manispaa ni makusanyo madogo licha ya kuwepo kwa vigezo vingi na kuagiza kuongeza umakini katika ukusanyaji wa mapato.

Baadhi ya wadau kupitia vitengo mbalimbali walioudhuria kikao hicho wamesema nguvu zinaitajika katika ukusanyanji wa mapato kwa wakati lakini pia matalajio yao ni kukusanya asilimia zaidi ya 100% .
