Buha FM Radio

Wafadhili kuing’arisha hospitali ya rufaa Kabanga

January 27, 2026, 1:26 am

Wageni na uongozi wa Hospitali ya Rufaa kabanga wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutembelea hospitalini hapo. Picha na Sharifat Shinji.

Uongozi wa hospitali ya Rufaa Kabanga imejidhatiti kuboresha miundombinu na mazingira ya kutolea huduma za afya pamoja na kutowa huduma bora kwa wannchi hii ni kutokana na ufadhili unaoendelea kufadhili katika hospitali hiyo.

Na; Sharifat Shinji.

Taasisi za Tweega Medica, AFAS foundation na Kabanga foundation zimetembelea hospitali ya Rufaa Kabanga iliyopo wilayani Kasulu na kukagua miradi inayoendelea kutekalezwa ikiwemo ujenzi wa majengo ya huduma mbalimbali za matibabu.

Matembezi hayo yamefanyika chini ya mlezi na mmiliki wa wa hospitali ya Rufaa Kabanga Mhashamu Baba Askofu Joseph Roman Mlola, Wageni kutoka Uholanzi na uongozi wa hospitali hiyo wakilenga kutathmini jinsi miradi inavyoendelea na kuongeza ufadhili katika hospitali hiyo.

Ni miongoni mwa miradi ya majengo yanayojengwa katika Hospitalli ya Rufaa Kabanga. Picha na Sharifat Shinji.

Aidha Mganga Mfawidhi wa hospitali (MOI) Daktari bingwa wa upasuaji Ndg. Peter Kitenyi amesema wafadhili hao wanalenga kuongeza na kuendelea kuifadhili hosipitali hiyo katika miundombinu ili kuleta mabadiliko makubwa katika utowaji wa huduma za matibabu.

“Leo tumetembelewa na wageni ambao ni wafadhili wetu kutoka Tweega Medica, AFAS foundation na Kabanga Foundation wageni hao ni kutoka Uholanzi ambao wameambatana na mmiliki na mlezi wa hospitali yetu Mhashamu Baba Askofu Mlola, malengo yao ni kuendelea kutoa misaada katika hospitali yetu” Amesema Dkt. Kitenyi.

Dkt. Kitenyi ameongezea kwa kueleza kuhusu miundombinu ambayo itafadhilliwa katika hospitali hiyo ni ujenzi wa Maabara kubwa ya kisasa inayotarajiwa kuanza kujengwa hivi punde, ujenzi wa nyumba za watumishi na majengo mengine ya huduma za kiafya  katika hospitali hiyo.

“Wafadhili hawa wanalenga kusaidia katika ujenzi wa Maabara kubwa ya Kisasa ambayo ipo mbioni kuanza kujengwa, nyumba za watumishi majengo mengine ambayo yanaendea kujengwa katika hospitali yetu hivyo tutakuwa na mabadiliko Makubwa katika Hospitali yetu” Amesema Dkt. Kitenyi.

Ni mradi wa jengo la wagonjwa linaloendelea kujengwa katika hospitali ya Rufaa Kabanga. Picha na Sharifat Shinji.

Hospitali ya Rufaa Kabanga ni miongoni mwa Hospitali kubwa katika Mkoa wa Kigoma ambayo inapatikana katika Wilaya ya Kasulu ikiwa chini ya kanisa Katoliki jimbo la Kigoma  ikiwa inatowa huduma zote kubwa zikiwemo huduma za kibingwa kwa magonjwa mbalimbali kama magonjwa ya ndani, magonjwa ya wanawake na magonjwa mengine ya binadamu.