Buha FM Radio
Buha FM Radio
January 27, 2026, 2:15 am

Wananchi waeleza furaha ya huduma za madaktari katika hospitali ya Rufaa Kabanga iliyopo wilayani Kasulu na kupongeza uongozi kwa kuendelea kuwaborishea huduma za afya.
Na; Sharifat Shinji
Hospitali ya Rufaa Kabanga iliyopo Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma imewaomba wananchi kujitokeza katika wiki ya huduma za kibingwa katika hosipitali hiyo ikilenga kuwasaidia wakazi wa Mkoa wa Kigoma wenye changamoto mbalimbali za kiafya ikiwemo upasuaji na huduma zingine.
Wito huo umetolewa na Dkt. Ezibon Midaho wakati akizungumza kwa niaba ya Mganga Mfawidhi (MOI) Dkt. Peter Kitenyi, ambapo ameesema Hospitali imepokea Madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Bugando mkoani Mwanza kwa ajiri ya kutoa huduma za kibingwa kuanzia tarehe 26 hadi 30 Januari.

Aida amesema huduma hizo zitatolewa kwa wananchi wote, ikiwemo wananchi wenye bima ya afya na wasio na bima ya Afya huku akiwapongeza wananchi ambao wanaendelea kufika kupata huduma mbalimbali za matibabu hospitalini hapo.
Kwa upande wao baadhi ya wanchi waliojitokeza katika huduma hizo akiwemo Bi.Nezia Ntioza na Mwl. Waziri Mkoma, wameishukuru hispitali ya Rufa Kabanga kwa kuendelea kutoa huduma bora huku wakionesha furaha hayo ya kupata huduama za matibabu kwa ubora na ufanisi wa juu.

Hospitali ya Rufaa Kabanga huandaa kampeni mbalimbali kwa ajili ya matibabu kwa wananchi, zipo kampeni za muda mfupi ambazo huamdaliwa kila mwezi na kampeni ambazo huandaliwa mwisho wa mwaka kwa ajili ya kurudisha kwa jamii kama ilivyofanyika wiki ya afya Kabanga tarehe 15 hadi 20 mwezi wa 12 mwaka 2025 ambapo walifanikiwa kufaikia zaidi ya wananchi 7 kutoka wilayani Kasulu.