Buha FM Radio
Buha FM Radio
January 5, 2026, 10:29 pm

Katika msimu huu wa kilimo baadhi ya wakulia wa kata ya Karela wamebainisha changamoto ambazo wamekuwa wakizipitia katika kila msimu wa kilimo katika maeneo hayo.
Na; Emily Adam
Wakulima wa kata ya Karela Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma wameshauriwa kufuata mbinu bora za kilimo ikiwemo kupanda , kupalilia na kuvuna kwa wakati ili kuongeza ubora na wingi wa mazao wakati wa uvunaji.
Wito huo umetolewa na Afisa kilimo wa kata ya hiyo Ndg. Leokaja Arufred wakati akizungumza na Buha FM Radio katika ofisi ya kijiji cha Karela juu ya mbinu muhimu wanazopaswa kutumia wakulima ili kuongeza thamani ya mazao yao.
Kwa upande wao baadhi ya wakulima wa kata ya Karela wamesema wamekuwa wakikumbana na changamoto kubwa ya ukosefu wa mitaji kwa ajili ya kuendesha shughuli ya kilimo huku wakati mwingine wakishindwa kabisa kulima eneo zaidi ya moja.
Awali Afisa Kilimo amesema wameaandaa mpango wa kuwafikia maafisa kilimo kuwauliza mbinu bora na za kisasa za kilimo ili kukabiliana na changamoto zinazowakabili ikiwemo mabadiliko ya hali ya hewa pamoja na mgaonjwa shanbulizi ya mimea.