Buha FM Radio
Buha FM Radio
January 5, 2026, 7:06 pm

Mbunge wa Kasulu vijijini Mhe. Edibily Kazala aneahidi kutatua changamoto zote ilizopo katika kijiji cha Kagerankanda na Jimbo la Kasulu vijijini kwa ujumla.
Na; Mwandishi wetu
Wananchi wa kijiji cha Kagerankanda katika Jimbo la kasulu Vijijini Mkoani Kigoma wamemuomba Mbunge wa jimbo hilo kutatua kero zilizopo ndani ya kijiji hicho ikiwemo mgogoro wa wakulima na wafugaji.
Malalamiko hayo wameyatoa jana kijijini hapo wakati wa mkutano wa hadhara wa mbunge wa jimbo hilo na kusema licha ya uwepo wa mgogoro huo bado kijiji hicho kinakumbwa na changamoto za huduma ya afya kutokana na wajawazito kutozwa fedha wakati wa kujifungua.
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo hilo Edibily Kazala ameahidi kutekeleza ahadi zote alizoziahidi katika kipindi cha kampeni ikiwa ni pamoja na kutatua migogoro ya ardhi hasa katika eneo la Katoto lililouzwa kinyume na taratibu za kisheria.
Aidha Mbunge huyo ameongeza kwa kusema ameanza mchakato wa kuhakikisha barabara za lami zilizopo katika mpango wa serikali zinajengwa na kukamilika kwa wakati ili kuinua uchumi wa wananchi wa kijiji hicho.
Sauti ya Mbunge wa Kasulu Vijijini Edibily Kazala.
