Buha FM Radio
Buha FM Radio
December 11, 2025, 12:33 pm

Mwanasheria kutoka kituo cha Matumani (Centre of Hope), kilichopo wilayani Kasulu Ndug. Decas Patrick Burumba amewaomba wazazi na walezi wa Wilaya ya Kasulu kuzingatia na kufuata sheria za haki za watoto na kuwalinda dhidi ya ukatili katika jamii.
Na; Helbeth Barayata
Wananchi wilayani Kasulu mkoani Kigoma wameshauriwa kuzingatia haki za mtoto kwa mujibu wa sheria ikiwa ni pamoja na haki ya Kulidwa, Kurithi, Kutoa maoni na kusikilizwa, kuelelewa na wazazi pamoja na mambo mengine yanayowahusu watoto.
Wito huo umetolewa na Mwanasheria kutoka kituo cha Matumani (Centre of Hope), kilichopo wilayani Kasulu Ndug. Decas Burumba wakati akizungumza na Buha FM radio Kupitia kipindi cha Darasa Nje ya shule na kusema kutozingatia haki hizo ni kumfanyia ukatili mtoto.
Aidha Burumba ameendelea kwa kusema iwapo haki za mtoto zitavunjwa kwa namna yoyote mhusika atachukuliwa hatua za kisheria kwa kupewa adhabu kulingana na kosa alilolifanya kutoka katika kifungu cha 14 hadi 16 cha sheria ya haki ya mtoto.

Mwanasheria huyo amebainisha kuwa kwa mjibu wa Katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania inatambua mtoto mwenye umri kati ya 0 hadi miaka 17, hata hivyo amendelea kwa kusema taratibu za kidini na kimira hazitambuliki kwa mjibu wa sheria za nchi.
Pamoja na kubainisha haki za mtoto amefafanua jinsi ya wazazi, walezi na jamii inavyopaswa kumlinda mtoto dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa kutoa taarifa katika vyombo vya Dola pale vitendo hivyo vinapogundulika.
Amehitimisha kwa kusema ili kutokomeza vitendo vya ukatili serikali ilianzisha tasisi ya SAMIA LEGAL AID FOUNDATION yenye lengo la kutoa msaada wa kisheria nchi nzima, na kuanzisha kitengo cha dawati la jinsia katika kila kata maeneo yote Nchini.