Buha FM Radio
Buha FM Radio
December 10, 2025, 4:45 pm

Wilaya ya Kasulu imeendelea kuimalika katika kutekeleza miradi inayoendelezwa na ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM kwa kuendeleza na kukikamilisha kwa usimamizi bora huku mingine ikiendelea kutekelezwa wilayani humo.
Na; Paulina Majaliwa
Serikali wilayani Kasulu mkoani Kigoma imeendelea kusimamia na kutekeleza miradi ya maendeleo, mbalimbali inayotekelezwa katika baadhi ya maeneo wilayani humo hali inayodhihirisha nguvu ya ushirikiano kati ya Serikali na wananchi.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya, katika kikao cha Kamati ya Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Kasulu cha kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha Julai hadi Novemba 2025 katibu tawala Wilaya ya Kasulu Bi. Theresia Mtewele, amesema serikali wilayani Kasulu imeendelea kuimarisha miradi hiyo na hali ya uwekezaji ikizidi kuimarika.
Aidha amesema Serikali ya wilaya ya Kasulu imeendeleza kutengeneza mahusiano mazuri na makundi mbalimbali ya jamii, kuanzia viongozi wa dini, vyama vya siasa, wafanyabiashara pamoja na taasisi binafsi na za kiserikali, jambo lililochochea utulivu katika kupanga na kutekeleza maendeleo ndani ya Wilaya.
“Serikali wilayani Kasulu imejitahidi kuweka mahusiano na makundi mbalimbali ikiwemo viongozi wa dini,vyama vya siasa a makundi mengine mengi hii ni moja wapo ya njia inayorahisisha utendaji kazi wetu ndani ya wilaya na mkoa wa kigoma kwa ujumla” Amesema Mtewele.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kasulu, Ndg. Mbelwa Abdallah, amewataka viongozi wa Serikali, wabunge na madiwani wa CCM kudumisha mahusiano mazuri na watendaji na wananchi wote ili kuleta mshikamano mzuri ndani ya jamii na nchi kwa ujumla.

Nao baadhi ya madiwani kutoka kata mbalimbali wilayani Kasulu wamewasilisha changamoto mbalimbali zinazowakabili katika kata zao nakuiomba serikali kutatua changamoto hizo kwa kukamilisha ujenzi wa miundombinu ambayo haijakamilika.