Buha FM Radio

Mbunge Kasulu Vijijini atoa maelekezo kwa madiwani

December 4, 2025, 6:19 pm

Mbunge wa Jimbo la Kasulu Vijijini Edibil Kazara wakati akiongea kwenye kikao cha kwanza cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu. Picha na Emily Adam.

Madiwani wa Kata mbalimbali katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu wamepewa maelekezo ya kufanya baada ya kula viapo vyao vya kuwatumikia wananchi katika kata zao.

Na; Emily Adam

Watumishi  wa sekata mbalimbali na Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma wamehimizwa kufanya kazi kawa ushiriano mkubwa ili kuhakikisha wanachochea kasi ya maendeleo pamoja kutatua kero mbalimbali zinazo wakabili wananchi katika maeneo yao.

Wito huo umetolewa na Mbunge wa Jimbo la Kasulu Vijijini Edibily Kazala wakati akiongea kwenye kikao cha kwanza cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Kagoma Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu.

Sauti ya Mbunge wa Jimbo la Kasulu Vijijini Edibily Kazala.

Aidha Mbunge huyo amesema Madiwani hawana budi kufanya kazi kwa kushirikiana na watumishi,na watalaam wa Halmashauri ya Wilaya ya Kusulu na  kuhakikisha wanatekeleza ahadi walizoziahidi kwa wananchi wakati wa kampeni ndani ya jimbo.

Sauti ya Mbunge wa Jimbo la Kasulu Vijijini Edibily Kazala.

Kwa upande wake Mbwelwa Abdallah ambaye ni mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Kasulu amewaasa madiwani hao kufanya kazi kama timu moja yenye moyo unaofanana na kujiepusha na makundi yanayoweza kuharibu taswira nzima ya Wilaya hiyo.

Sauti ya mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kasulu Mbwelwa Abdallah.

Hata hivyo mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Samwel Filbert Kadogo akiongea kwa niaba ya Madiwani hao amesema watahakikisha wanafanya kazi kwa kutanguliza masilahi ya wananchi na jamii kwa ujumla ndani ya kipindi cha miaka mitano.