Buha FM Radio

Kasulu waomba nyama ishuke bei msimu wa sikukuu

December 3, 2025, 5:51 pm

Mmoja ya wafanyabiashara ya nyama katika soko la Mnadani. Picha Helbeth Barayata.

Wafanya biashara wa nyama katika Halmashauri ya Mji Kasulu wameeleza namana soko la nyama linavyoendelea pamoja na kubainisha kuwa bei ya nyama kupanda ni kutokana na soko la ng’ombe kuwa juu.

Na; Sharifat Shinji

Wafanya biashara wa nyama katika soko la Mnadani Halimashauri ya Mji Kasulu Mkoani Kigoma wameeleza hali ya upatikanaji wa nuyama na bei yake kwa sasa kuelekea msiku wa sikuku ya krisimas na mwaka mpya.

Wakizungumuza na Buha FM Radio kwa nyakati taofauti wamesema upatikanaji wa nyama upo vizuri ukilinganishwa na idadi ya wateja wanaohitaji huduma hiyo, na kubainisha kuwa tangu July mwaka huu bei ya nyama ya Ng’ombe ilipanda kutoka 10,000/= mpaka 11,000/= kwa kilo moja (1kg).

Sauti ya wafanya biashara ya nyama.

Aidha Bi Sabina Mssa ni mkazi wa mnadani amezungumza kwa niaba ya wateja na kukiri  kuwa upatikanaji wa nyama hauna shaka akiomba punguzo la bei amebainisha kwa  kusema awali walikua wakinunua kwa 9,000/= mpaka 10,000/= lakini kwa sasa nyama imepanda na kufikia shilingi 11,000/=  hadi 12,000/=

Sauti ya Bi Sabina Mssa mkazi wa mnadani.

Hata hivyo wafanyabiashara wa nyama wamefafanua sababu za bei ya nyama kupanda ni kutokanana na soko la mifugo kuwa juu hali iliyopelekea  bei ya nyama kupanda na kuwaomba wateja kuendana na hali iliyopo kwa sasa, japo wateja wameomba kupunguzwa kwa bei katika msimu huu wa kuelekea sikuku ili kuwezesha kumudu gharama yake.