Buha FM Radio
Buha FM Radio
December 3, 2025, 1:06 pm

Baadhi ya wananchi wa maisha ya chini wamewaomba Wafanyabiashara wa Mchele katika masoko ya Halamashauri ya Mji Kasulu kupunguza bei ya bidhaa hiyo kutokana na gharama kupanda na baadhi ya wananchi kushindwa kumudu gharama hizo.
Na; Emily Adam
Wafanyabiashara wa mchele Wilyani Kasulu Mkoani Kigoma wameeleza hali ya upatikani wa bidhaa hiyo kuwa sio rahisi hali inayowalazimu kuuza kwa bei ya juu licha ya kuendelea kulalamikiwa na wateja wao ambapo kwa sasa mchele unauzwa kwa wastani wa 2000/= hadi 2600/= kwa kilo kimoja (kg1).
Wamebainisha hayo wakati wakizungumza na Buha FM Radio juu ya hali ya kupanda kwa bei ya mchele ghafla wilayani humo, baadhi ya wafanya biashara hao akiwemo Nuhu Leonard na Paskali Ndayahande kutoka wamesema bei hiyo ni kutokana na bidhaa hiyo kuwa adimu kupatikana.
Aidha wamewaasa wafanya bishara wakubwa wa jumla wa Mchele kuwa waaminifu na kucha tabia ya baadhi yao kutokuwa waaminifu kwa kuchanganya Mchele mbovu na mzuri hali ambayo imekuwa ikiwaumiza na kuwapa hasara wateja wao.
Kwa upande wao baadhi ya watumiaji wa mchele Wilyani Kasulu wamesema kutokana na ongezeko hilo la bei wanalazimika kununua kwa bei hiyo na kupunguza ratiba za kula wali badala yake hulazimika kununua chakula chenye bei rahisi kama vile viazi,ndizi na mahindi kutokana na hali duni ya maisha.
Kwa kawaida ilivyo zoeleka nchini tanzania katika soko la mchele ifikapo mwezi Novemba hadi Februri mchele hupanda kutokana na muda huo soko la Mpunga huwa ni gumu kupatikana pia mahitaji huwa ni makubwa kutokana na sikukuu za mwisho wa mwaka.