Buha FM Radio

Kasulu waomba kupewa elimu kuhusu UKIMWI

December 2, 2025, 11:19 pm

Dkt. Damas chibeta, kutoka Hospitali ya Mlimani Halmashauri ya Mji wa Kasulu baada ya mahojiano na mwandishi wa Buha FM Radio. Picha na Irene Charles.

Wakazi wa Wilaya ya Kasulu waombwa kujenga utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara na kutambua mapema kama wanaishi na maambukizi ya virus vya UKIMWI ili kupata ushauri nasaaha pamoja na kuanza matumizi ya kufubaza maambukizi ya virusi hivyo.

Na; Irene Charles

Baadhi ya Wananchi na Wakazi wa Halmashauri ya mji Kasulu mkoani Kigoma wameiomba serikali kuendelea kutoa elimu ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI, huku wakisema bado kuna uhitaji mkubwa wa lkupewa uelewa juu ya janga hilo.

Wakizungumza na Buha FM Radio, katika Siku ya maadhimisho ya UKIMWI Duniani, wananchi hao wamesema serikali pamoja na wadau mbalimbali wanatakiwa kuongeza jitihada ya utoaji elimu katika jamii kwani hapo zamani ilikuwa inatolewa kwa kiwango cha juu tofauti sasa.

Sauti za wananchi.

Kwa upande wake, Dkt. Damas chibeta, kutoka Hospitali ya Mlimani Halmashauri ya Mji wa Kasulu amesema kuishi na mtu mwenye maambukizi ni salama kabisa kwa kufuata muungozo na sio kwa kuwanyanyapaa kwani kufanya hivyo ni kuwatesa kisaikolojia.

Aidha Dkt Damas amewashauri wananchi kupima mara kwa mara, kutochangia vitu vyenye ncha kali,kutumia kinga, kutumia dawa za kuzuia maambukizi pamoja na kuepuka ngono zembe ni njia za kujikinga UKIMWI.

Sauti ya Dkt. Damas chibeta, kutoka Hospitali ya Mlimani Halmashauri ya Mji wa Kasulu.

Dkt Damas amesema kupungua uzito, kukosa nguvu, homa za mara kwa mara, joto kali usiku, kuhara kwa muda mrefu ni dalili ambazo zinaashiria maambukizi ya UKIMWI.

Sauti ya Dkt. Damas chibeta, kutoka Hospitali ya Mlimani Halmashauri ya Mji wa Kasulu.

Kwa mujibu wa Kaimu mkurugenzi mtendaji wa tume ya kuthibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dkt. Samweli Sumba amesema kulingana na utafiti wa mwaka 2022/2023, Tanzania inakadidiwa kuwa na watu 1,700,000 wanaoishi na virusi vya ukimwi kati yao, zaidi ya watu 1,500,000 wako kwenye huduma za matibabu na matunzo.