Buha FM Radio

Zimamoto: Majanga ya radi si ushirikina

November 28, 2025, 12:05 am

Mkuu wa Jeshi la Zimamaoto Wilaya ya Kasulu, Mrakibu Msaidizi Antony Marwa akitoa maelezo kuhusu majanga ya moto na uokoaji kwa watumishi wa Halamashauri ya Mji Kasuli. Picha na Sharifat Shinji.

Watumishi wa Halimashauri ya Mji Kasulu wamepewa elimu ya kujikinga na majanga ya moto pamoja na mbinu za kutumia vifaa vya uokozi ikiwemo vizima moto pamoja na hatua za kuchukuwa pale wanapofikwa na majanga katika maenoe yao ya kazi.

Na; Sharifat Shinji

Jeshi la Zimamoto Wilaya ya Kasulu limetoa elimu ya kutumia vifaa vy uokozi na vizima moto kwa watumishi wa Umma katika Halmashauri ya Mji Kasulu lengo likiwa kuwasaidia kutambua namna ya kujiokoa na majanga ya moto yanayoweza kujitokea.

Akizungumza baada ya mafunzo hayo Mkuu wa Jeshi la Zimamaoto Wilaya ya Kasulu, Mrakibu Msaidizi Antony Marwa amesema kutokana na ongezeko la majanga ya moto katika maeneo mengi wameamua kutoa elimu kwa watumishi wa Halmashauri ya Mji Kasulu ili kulahisisha ufikiwaji wa elimu kwa wananchi.

Sauti ya Mkuu wa Jeshi la Zimamaoto Wilaya ya Kasulu, Mrakibu Msaidizi Antony Marwa.

Aidha Mkurugenzi wa Halmashauri  ya Mji Kasulu Mwl. Vumilia Simbeye amesema lengo la kupewa elimu kwa watumishi hao ni kutokana  na baadhi yao kutokuwa na uelewa wa matumizi sahihi ya vifaa vya kuzima moto huku akibainisha mpango wa halmashauri kuwafikia wananchi wa kwaida kwa ajili ya elimu hiyo.

Sauti ya Mkurugenzi wa Halmashauri  ya Mji Kasulu Mwl. Vumilia Simbeye.
Mkurugenzi wa Halmashauri  ya Mji Kasulu Mwl. Vumilia Simbeye akieleza namna mafunzo hayo yalivyowawezesha watumishi kutambua matumizi na jia mbalimbali ya kujisaidia na majanga ya moto. Picha na Sharifat Shinji.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Jeshi la Zimamaoto amesema wananchi waache nadharia ya kuhusisha majanga ya moto na imani za kishirikina huku akiwasii wananchi kuachana na vitendo vya kuhifadhi vitu hatarishi ndani vinavyoweza kusababisha milipuko ya Moto.

Sauti ya Mkuu wa Jeshi la Zimamaoto Wilaya ya Kasulu, Mrakibu Msaidizi Antony Marwa.
Mkuu wa Jeshi la Zimamaoto Wilaya ya Kasulu, Mrakibu Msaidizi Antony Marwa akitoa maelezo kuhusu majanga ya moto na uokoaji kwa watumishi wa Halamashauri ya Mji Kasuli. Picha na Sharifat Shinji.

Kwa upande wao baadhi ya watumishi na wanufaika wa mafunzo hayo wamelishukuru Jeshi la Zimamoto kwa msaada wa kielimu huku wakitaja baadhi ya mambo waliyojifunza kutoka katika Jeshi hilo la uokozi.

Sauti ya baadhi ya watumishi na wanufaika wa mafunzo hayo.
Baadhi ya watumishi na wanufaika wa mafunzo hayo wakifatilia maelezo kutoka Jeshi la Zimamaoto. Picha na Sharifat Shinji.

Jeshi la Zimamoto na uokoaji linaendelea kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ili kuwezesha wananchi kupata uelewa juu ya matumizi mbalimbali ya vifaa vya uokozi na jinsi ya kujikinga na majanga ya moto na majanga mengine huku mkuu huyo akiwaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikianao kwa kupiga simu bure kwenda namba 114 kwa ajili ya msaada wa uokozi pale yanapotokea majanga.