Buha FM Radio

World Vision yazifikia shule za Tulieni na Chashenze Kasulu

November 26, 2025, 11:02 pm

Mratibu wa Shirika World Vision Tanzania kwa Wilaya ya Kasulu, Ester Mushendwa,akisoma taarifa ya mradi mbele ya mgeni Mkuu wa Wilaya. Picha na Sharifat Shinji.

Wazazi na walezi katika kata ya Makele Tarafa ya Makele katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma wamepongea kukmilika wa ujenzi wa madarasa na matundu ya vyoo katika shule za msingi Tulieni na Chashenze katikakatika halimashauri hiyo, mradi uliotekelezwa na shirika la World Vision Tanzania.

Na; Sharifat Shinji

Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Mhe. Kanali Isaack Mwakisu, amelipongeza Shirika la World Vision Tanzania kwa mchango wake wa utekelezaji mirandi ya maendeleo ikiwemo elimu baada ya kukamilisha ujenzi wa madarasa manne na matundu 10 ya vyoo katika Shule za Msingi Tulieni na Chashenze katika Halamashauri ya Wilaya ya Kasulu.

Akizungumza wakati hafla ya makabidhiano yaliyofanyika, katika Shule ya Msingi Tulieni, Kata ya Makere, amesema mchango wa Shirika hilo wa kukamilisha ujenzi wa madarasa hayo utaleta tija katika serikali na kuwahamasisha wanafunzi kusoma kwa bidii kutokana na miundombinu bora ya kujifunzia.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Mhe. Kanali Isaack Mwakisu.
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Mhe. Kanali Isaack Mwakisu akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mradi wa madarasa katika shule ya msingi Tulieni. Picha na Sharifat Shinji.

Aidha Mwakisu amemtaka Mkuu wa shule hiyo kuhakikisha analinda miundombinu hiyo ili iweze kutumika kwa muda mrefu huku akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, CPA Francis Kafuku ya kuhakikisha anafuatilia na kukagua miradi hiyo na kuwaonya wanafunzi juu ya vitendo vya kujihusisha na uharibifu wa miundombinu.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Mhe. Kanali Isaack Mwakisu.

Katika hatua nyingine Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Tulieni, Ayubu Ugasa, amelishukuru shirika la World Vision kwa kuwakamilishia vyumba vya madarasa na kuahidi kutunza miundombinu hiyo kama ilivyoelekezwa, huku madarasa hayo yatawasaidia wanafunzi 484 wa shule ya Tulieni.

Suti ya Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Tulieni, Ayubu Ugasa.

Awali akisoma taarifa ya mradi mbele ya mgeni Mkuu wa Wilaya, Mratibu wa Shirika World Vision Tanzania kwa Wilaya ya Kasulu, Ester Mushendwa, amesema mradi huo wa madarasa umegarimu zaidi ya milioni 200 za Kitanzania ambapo utawanufaisha wanafunzi 764 wavulana 375 na wasichana 389.

Sauti ya Mratibu wa Shirika World Vision Tanzania kwa Wilaya ya Kasulu, Ester Mushendwa.
Mratibu wa Shirika World Vision Tanzania kwa Wilaya ya Kasulu, Ester Mushendwa,akisoma taarifa ya mradi mbele ya mgeni Mkuu wa Wilaya. Picha na Sharifat Shinji.

Bi. Mushendwa amemalizia kwa kusema shirika limeendelea na zoezi la utoa ji elimu pia shirika limefanya ukaguzi wa vyoo  katika Kaya zaidi ya 3000  za kata  mbalimbali za Halmashauri ya Wilaya Kasulu na kubaini idadi kubwa ya Kaya kuwa na ukosefu wa vyoo bora huku wakiwezesha kujengwa vyoo zaidi ya 1000 katika kata hizo.

Sauti ya Mratibu wa Shirika World Vision Tanzania kwa Wilaya ya Kasulu, Ester Mushendwa.
Mkuu wa mkoa akiwa kwenye picha na wanafunzi wa shule ya msingi Tulieni katika kata ya Makere. Picha na Sharifat Shinji.

Nao baadhi ya  wazazi wa wanafunzi  katika shule ya Tulieni wameshukuru kwa kukamilishiwa madarasa hayo na kusema utawaaidia watoto kuhudhulia shuleni kutokana na miundombinu bora ya kujifunzia.

Sauti za baadhi ya wazazi wa wanfunzi wa shule ya msingi Tulieni.

Shirika la World Vision Tanzania ni shirika la kikisriso linalodhaminiwa na serikali ya Marekani limenza kufadhili miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mwaka 2010 na linatarajiwa kumaliza ufadhili wake mwaka 2026, likiwa limefadhili miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo masuala ya elimu, afaya, miundombinu, kilimo na maswala ya ulizi kwa watoto dhidi ya ukatili wa kijinsia.